Taarifa Rasmi.
Matokeo ya supplimentary yanatarajiwa kutolewa tarehe 28 september kwa mujibu wa almanac ya chuo chetu, hivyo basi ni siku mbili tu zimebaki kuanzia sasa ili matokeo hayo yatolewe.
Tuendelee kuomba Mungu ili matokeo yawe mazuri kwa kila mmoja wetu.
Kama kuna tatizo/ shida fika ofisi ya COBESO tukuhudumie.
Tuesday, 26 September 2017
Monday, 18 September 2017
TAHLISO YAITAKA HESLB KUTOA NAFASI YA MAREKEBISHO KWA WANAFUNZI WALIOKOSEA KUJAZA FOMU ZA KUOMBA MKOPO.
Ni siku takribani 6 sasa zimepita tangu Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) wafunge dirisha la maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa wanaotarajia kujiunga na masomo ya vyuo vikuu pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ya elimu ya juu waliokosa mkopo mwaka wa jana 2016/2017 wanaoishi katika mazingira magumu.Mpaka sasa tunatambua kwamba mchakato wa kuwachambua wote walioomba ili kuweza kujua idadi kamili ya walioomba mkopo bado inaendelea, jambo ambalo litabainisha idadi ya wanafunzi walioomba kwa usahihi wa taarifa zao bila kukosea na pia kubainisha idadi ya wanafunzi waliokosea kujaza taarifa zao wakati wa kujaza fomu hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na bodi ya mikopo tarehe *30 August, 2017*ilidai mpaka kufikia tarehe hiyo walioomba walikuwa wanafunzi *49,282* na kati yao idadi ya wanafunzi *15473* ndio walijaza sahihi taarifa zao na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi waliokosea taarifa zao kuwa *33,809*
Nidhahiri idadi hiyo ya waliokosea yawezekana ikawa imeongezeka ama kubaki kama ilivyo kutokana na elimu iliyoendelea kutolewa na HESLB.
*TAHLISO* tunaiomba HESLB itoe nafasi kwa wale wote waliokosea kujaza fomu hizo ili waweze kufanya marekebisho hayo kwasababu kuna uwezekano mkubwa hao waliokosea ndio wenye uhitaji mkubwa kuliko waliopatia ujazaji wa fomu hizo kutokana na kuishi katika mazingira magumu ya maisha kiasi cha kushindwa hata kumudu matumizi ya kimtandao.
Ili kuepuka kuwaacha walengwa wenye uhitaji ndani ya kundi hilo la watu 33,809 *TAHLISO* tunaiomba *HESLB* Iliangalie hilo kwa jicho la pili ili kuwapa nafasi kwa mara nyingine ya kufanya marekebisho hayo ili kuweka usawa katika kuwajali watoto wa Maskini.
*STANSLAUS PETER KADUGALIZE MWENYEKITI TAHLISO*

Subscribe to:
Posts (Atom)