Raisi wa Serikali ya Wanafunzi CBE Dodoma Mhe, Brian L. Kifanga akipeana mkono na Meneja wa GEPF Kanda ya Kati Mr. Josephat Mshana wakati wa Makabidhiano ya vifaa vya Usafi vilivyotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii GEPF kwa kushirikiana na Serikali ya wanafunzi COBESO Dodoma ikiwa ni sehemu ya Kuunga Mkono Sera ya Mhe, Raisi wa Serikali ya Wanafunzi CBE Juu ya Uhifadhi wa Mazingira pamoja na kuwa na Mazingira safi. Makabidhiano hayo yalifanyika siku ya Ijumaa Tarehe 10 Mwezi wa 11. 2017 Katika Chuo cha elimu ya Biashara Dodoma.
Makabidhiano hayo yalishirikisha Baadhi ya Staff Kutoka GEPF Pamoja na Staff Kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara Dodoma na Viongozi kutoka serikali ya wanafunzi chini ya wizara ya Afya, Mazingira na Jinsia.
Kama Serikali ya Wanafunzi Tunapongeza Jitihada zilizofanywa na Wizara Husika pamoja na GEPF Kwa ajili ya Vifaa hivyo ambavyo vitaongeza tija katika Chuo chetu.
Imetolewa na;
Dadil C.M
Naibu waziri wa Habari na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment