Wednesday, 22 November 2017

Diploma II CAC League 2017

Wanachuo wa Diploma II wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea Ufunguzi wa Ligi ya Chuo Ijulikanayo kama CAC League 2017..

Katika Mechi ya Ufunguzi iliyochezwa Siku ya tar 21 Nov 2017 wanafunzi  wa Diploma II Waliibuka na Ushindi Mnono wa Goli 4 dhidi ya Bachelor 1

CAC League 2017


Wanachuo wa Bachelor 1 wakiwa kwenye maandalizi ya Mechi ya Ufunguzi wa Ligi ya Chuo ijulikanayo kama COBESO Annual Competition League (CAC League) 2017.

Katika Mechi hiyo wanafunzi wa Bachelor 1 walipokea kipigo cha Goli 4-1 Kutoka kwa Diploma II

Monday, 20 November 2017

Mahafali 2017


Wanachuo wa Diploma Wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kutunukwa stashahada zao, tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 18.11.2017 Siku ya Jumamosi katika mahafali ya 52 ya chuo cha Elimu ya Biashara campus ya Dodoma. 

Sherehe hiyo ya Mahafali ya 52 ya chuo cha Elimu ya Biashara ilihudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini, pamoja wageni kutoka sehemu mbalimbali pamoja na wandishi wa Habari...

Imetolewa na;

Dadil C.M
Naibu waziri wa Habari na mawasiliano
COBESO 2017/18

Friday, 17 November 2017

COBESO Dodoma News

I am Highly esteemed to welcome you to the second issue of COBESO Dodoma Campus, this issue presents some events and current success of COBESO with the goal of informing others on the development of COBESO Dodoma.

As you take time to read and pass through this issue let us continue to support COBESO for the walfare of the students and excellence..


Regards!  

DADIL C.M
Deouty Minister of information and Communication.
COBESO 2017

Wednesday, 15 November 2017

GEPF and COBESO Dodoma


Baadhi ya Viongozi wa serikali ya wanafunzi katika Picha ya pamoja na viongozi kutoka GEPF na Staff kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara mara baada ya tukio la makabidhiano ya vifaa vya Usafi wa Mazingira.. 

Vifaa vilivyotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF Kupitia wizara ya Afya, Mazingira na Jinsia kwa Ajili ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dodoma.

Imetolewa na;

Dadil C.M
Naibu waziri wa Habri na Mawasiliano

Makabidhiano ya Vifaa vya Usafi


Raisi wa Serikali ya Wanafunzi CBE Dodoma Mhe, Brian L. Kifanga akipeana mkono na Meneja wa GEPF Kanda ya Kati Mr. Josephat Mshana wakati wa Makabidhiano ya vifaa vya Usafi vilivyotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii GEPF kwa kushirikiana na Serikali ya wanafunzi COBESO Dodoma ikiwa ni sehemu ya Kuunga Mkono Sera ya Mhe, Raisi wa Serikali ya Wanafunzi CBE Juu ya Uhifadhi wa Mazingira pamoja na kuwa na Mazingira safi. Makabidhiano hayo yalifanyika siku ya Ijumaa Tarehe 10 Mwezi wa 11. 2017 Katika Chuo cha elimu ya Biashara Dodoma.

Makabidhiano hayo yalishirikisha Baadhi ya Staff Kutoka GEPF Pamoja na Staff Kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara Dodoma na Viongozi kutoka serikali ya wanafunzi chini ya wizara ya Afya, Mazingira na Jinsia.

Kama Serikali ya Wanafunzi Tunapongeza Jitihada zilizofanywa na Wizara Husika pamoja na GEPF Kwa ajili ya Vifaa hivyo ambavyo vitaongeza tija katika Chuo chetu.


Imetolewa na;

Dadil C.M
Naibu waziri wa Habari na Mawasiliano