
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)-mshindi wa tuzo ya chuo bora cha mwaka 2016 Tanzania, anawakaribisha waombaji (applicants) wenye sifa za kujiunga na chuo muhula mpya wa masomo mwezi wa Machi, 2018 na mwezi Septemba 2018 kwa programu za kutwa na jioni katika ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma), na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika kozi mbalimbali.
Programu hizi zinatolewa katika kampasi zote za chuo kama ifuatavyo:
A. ASTASHAHADA (CERTIFICATE PROGRAMMES) NTA LEVEL 4 (MWAKA 1)
1. Uhasibu (Accountancy)
2. Usimamizi wa Biashara (Business Administration).
3. Masoko (Marketing)
4. Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Management)
5. TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) (Dsm na Dodoma Pekee)
6. Mizani na Vipimo (Certificate in Metrology and Standardization) (Kwa Dsm Pekee)
Sifa za Kujiunga
1. Mwombaji awe amemaliza kidato cha NNE (IV) na kupata ufaulu wa angalau masomo 4 kwa kiwango cha kuanzia D (4D’s).
Zingatia: Muombaji wa kozi ya Uhasibu anapaswa awe amefaulu (Form IV) Hesabu kuanzia kiwango cha D. Na anaeomba Kozi ya Mizani na Vipimo awe amefaulu Hesabu au Fizikia kuanzia kiwango cha D.
AU
2. Awe amesoma na kuhitimu NABE II kwa ufaulu wa angalau alama 4
Ada ya Masomo
Ada ya masomo kwa Mwaka ni TZS 920,000/= isipokuwa kwa kozi ya TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) ambayo ada yake ni Tshs. 1,220,000/= na Mizani na Vipimo (Certificate in Metrology and Standardization) ambayo ada yake ni Tshs. 853,000/=
B. STASHAHADA (DIPLOMA PROGRAMMES) NTA LEVEL 5 – 6 (MIAKA 2)
1. Stashahada ya Uhasibu (Diploma in Accountancy)
2. Stashahada ya Usimamizi wa Biashara (Diploma in Business Administration)
3. Stashahada ya Ununuzi na Ugavi (Diploma in Procurement and Supplies)
4. Stashahada ya Masoko (Diploma in Marketing)
5. TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) (Dsm na Dodoma Pekee)
6. Mizani na Vipimo (Diploma in Metrology and Standardization) (Dsm Pekee)
Sifa za Kujiunga
1. Mwombaji awe amemaliza kidato cha SITA (VI) na kupata ufaulu wa angalau Principal Pass Moja au Subsidiary Mbili katika masomo unganishwa (Combination subject). AU
2. Awe amesoma na kuhitimu Astashahada (Certificate) kutoka chuo kinachotambulika na NACTE katika fani zifuatazo:
· Usimamizi wa Biashara (Business Administration).
· Masoko (Marketing)
· Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Management)
· TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT)
Ada ya Masomo
Ada ya masomo kwa Mwaka ni TZS 1,100,000/= isipokuwa kwa kozi ya TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) ambayo ada yake ni Tshs. 1,400,000/= na Mizani na Vipimo (Diploma in Metrology and Standardization) ambayo ada yake ni Tshs. 1,014,400/=
C. STASHAHADA YA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA PROGRAMMES)
1. Postgraduate Diploma in Project Management (PGDPM) – Mwanza pekee
2. Postgraduate Diploma in Business Administration PGDBA) – Mwanza pekee
3. Postgraduate Diploma in Human Resource Management (PGDHRM) – Mwanza pekee
4. Postgraduate Diploma in Financial Management (PGDFM) – Mwanza pekee
5. Postgraduate Diploma in Investment (PGDIn) – Mwanza pekee
Ada ya Masomo:
Ada ya masomo kwa Mwaka ni TZS 1,800,000/=
Sifa za kujiunga na Postgraduate Diploma (PGD)
1. Mwombaji awe amehitimu Shahada (Degree) au Stashahada ya juu (Advanced Diploma). AU
2. Mwombaji awe na CPA au CPSP
D. UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI/KUJIUNGA NA CHUO
Maombi yote ya kujiunga na chuo yanafanyika chuoni au kwa njia ya mtandao (Online Application) kupitia tovuti ya chuo www.cbe.ac.tz kwa gharama ya TZS 10,000 tu.
Chuo kimepata kuwa chuo bora cha mwaka kwa mwaka 2016. Njoo ujiunge na chuo bora kwa elimu bora.
ZINGATIA:
Ada italipwa kwa awamu nyingi kama itakavyo elekezwa. Hostel zipo kipaombele kitatolewa kwa watakaowahi kuja kuanza masoma.
E. MAHALI TULIPO
2 Dodoma
Eneo la Makole pembezoni mwa barabara iendayo Dar es Salaam
S. L. P. 2077, Dodoma
Website:cbe.ac.tz/dodomacampus